CHANZO CHA KUTOAJIRIWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU

Kwa miaka mingi taasisi za elimu ya juu zimekuwa zikinyooshewa vidole kwa kushindwa kuzalisha wahItimu wanaoweza kukidhi mahitaji ya soko la ajira.  Taasisi hizi zimekuWa zikilaumiwa kwa kutoa elimu iliyojaa nadharia zaidi ambayo kimsingi inaonekana haitoshi kumjenga muhitimu ili aweze kumudu mahitaji ya soko la ajira lililojawa na ushindani.

Hivi karibuni Chama cha Waajiri Afrika Mashariki kupitia Dk Aggrey Mlimuka na Mwenyekiti wake Rosemary Ssenabulya kimeeleza kuwa nusu ya Wahitimu wa vyuo vikuu Afrika Mashariki hawana ujuzi na sifa za kuajirika.

Kauli hii inalandana na ripoti ya Shirikisho la Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki (IUCEA) iliyotolewa na mwaka 2014. Ripoti hii inaonyesha katika nchi za Afrika Mashariki, vyuo vikuu vya Uganda vinaongoza kwa kutoa wahitimu ambao hawajapikwa vya kutosha kukidhi mahitaji ya soko la ajira. Asilimia 63 ya wahitimu wa vyuo vya Uganda hawakidhi mahitaji ya soko ikifuatiwa na Tanzania ambayo 61% ya wahitimu wake wanatatizo hilo pia. Burundi ni asilimia 55 huku Rwanda ni asilimia 52 na Kenya asilimia 51.

Kwa matokeo ya ripoti hii kwa lugha nyingine ni sawa na kusema kati ya wanafunzi 100 wanaohitimu elimu ya juu nchini 61 hawana sifa stahiki zinazohitajika na waajiri au soko la ajira kwa ujumla. Hii haileti mrejesho mzuri juu ya mfumo wetu wa elimu.

CHANZO NI NINI?

Pamoja na lawama zinazotolewa kwenye taasisi za elimu ya juu bado kuna haja ya kuangalia mfumo mzima wa elimu. Ikumbukwe kuwa mara nyingi taasisi za elimu ya juu ni mdau wa mwisho katika mchakato wa kumpika mwanafunzi kabla hajaenda kwenye soko la ajira. Tuanze kwa kuhoji ubora wa elimu wanayopata wanafunzi kabla ya kuingia kwenye taasisi za elimu ya juu. Je, wanapata msingi mzuri wa maarifa na ujuzi wanapopitia katika shule za awali, msingi na sekondari?

Hivi karibuni Raisi mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania, Benjamin Mkapa amenukuliwa akieonyesha kusikitishwa na kiwango cha ubora wa mfumo wetu wa elimu kiasi cha kupendekeza mdahalo wa kitaifa kujadili masuala ya elimu.

Kumekuwa na changamoto nyingi zinazohusiana na ubora wa elimu kwenye shule za msingi na sekondari ambazo ndiyo daraja la kuwafikisha wanafunzi hawa kwenye taasisi za elimu ya juu.

Pamoja na hayo taasisi za elimu ya juu haziwezi kuepuka lawama za uzalishaji wa wahitimu butu kwani taasisi nyingi zimekuwa zikiendeshwa kibiashara bila kujali ubora wa elimu inayotolewa. Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekuwa ikionyesha jitihada kwa kuzuia udahili kwa baadhi ya kozi kwenye baadhi ya vyuo huku vingine vikilazimika kufungwa kwa kukosa vigezo stahiki vya kuzalisha wahitimu wenye sifa.

Ikumbukwe pia taasisi hizo hizo zilizoonekana kuwa na mapungufu pengine zimeshazalisha wahitimu wengi walioko kwenye soko la ajira hivi sasa. Hii inatoa tafsiri kuwa bado kuna safari ndefu ya kuboresha taasisi za elimu  na elimu kwa ujumla. Lawama zimekuwa nyingi na za kuondoa imani juu ya taasisi zetu kiasi cha wadau wengine kusema wahitimu wa taasisi hizi hawawezi hata kujieleza wakaeleweka huku wengine hawana uwezo hata wakuandika barua rasmi.

 

NINI KIFANYIKE?

Kuna haja ya kupitia upya mfumo wetu wa elimu na kuhakikisha kuwa unamifumo na mazingira wezeshi ya kuwajenga wanafunzi katika kupata maarifa na ujuzi. Hii inaanzia kwa kuwa na walimu na wakufunzi wenye sifa stahiki na miundombinu bora.

Taasisi za elimu ya juu zinatakiwa zifanye tafiti za kutosha kujua mahitaji ya soko la ajira na kuandaa mitaala inayokidhi mahitaji hayo. Hii iendane sambamba na kuongeza mafunzo kwa vitendo ili kuwajengea uwezo wa kutosha wanafunzi katika taasisi hizi.

Nje ya elimu inayotolewa kupitia mitaala ya elimu taasisi za elimu zinapaswa kubuni pogramu mbali mbali zitakazowawesha wanafunzi kupata ujuzi na maarifa ambayo masomo ya darasani hayawezi kutoa.

Kwa kuzingatia takwimu za IUCEA zinazoonesha kuwa asilimia 61 ya wahitimu wa vyuo vikuu hawana ujuzi na maarifa stahiki tunapata picha kuwa kuna asilimia nyingine 49 ambayo haipo kwenye kundi hili. Swali la kuhoji ni je, hawa asilimia 49 wanaobaki wanapita katika mfumo upi wa elimu? Majibu yanaweza kutofautiana, sababu zinaweza kuwa pengine baadhi ya wahitimu wamepitia shule zinazoaminika kutoa elimu bora kuliko wengine. Lakini pia kuna shuhuda za wanafunzi waliopitia kwenye mfumo huu unaonekana kuwa na changamoto nyinig lakini wakafanikiwa kujitofautisha na kuhitimu wakiwa na sifa stahiki zinazohitajika na soko la ajira.

Hii inatoa tafsiri kuwa ubora wa muhitimu unasababishwa na mambo mengi ikiwemo jitihada za muhitimu mwenyewe hasa alipokuwa kwenye mfumo wa elimu na baada ya kuhitimu pia. Wanafunzi wanatakiwa kujifunza mbinu za kuboresha uwezo wao na kujitofautisha na wengine. Hii inajumuisha kutafuta fursa za kujitolea ili kujiongezea ujuzi zaidi na kuwa tayari kujifunza katika mfumo usio rasmi.

Pia, wanafunzi wanatakiwa kutotegemea kile wanachokipata darasani pekee kwani mara nyingi uwa hakitoshelezi katika kutengeneza wahitimu wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira. Kutafuta taarifa kwenye vitabu, intaneti, kuhudhuria makongamano na kujifunza kutoka kwa wale waliofanikiwa kwenye fani husika kunaweza kusaidia katika kuwajenga wanafunzi na hivyo kuhitimu wakiwa na uwezo na sifa zinazohitajika.

Wizara ya elimu pia iwe tayari kutafuta, kupokea na kufanyikia kazi mapendekezo ya wadau mbali mbali juu ya namna ya kuboresha mfumo wa elimu kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika mfumo wa elimu yatakayowezesha uzalishaji wa wahitimu wenye ujuzi, marifa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya soko la ajira.

Facebook Comments

289 thoughts on “CHANZO CHA KUTOAJIRIWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU

 1. CartezDop

  coronavirus patent
  [url=http://chloroquine-cureforcoronavirus.com/#]coronavirus bht cure
  [/url] coronavirus kansas
  chloroquine
  – coronavirus location
  coronavirus mers

  Reply
 2. DennOl

  but there are also medicate worthless generic viagra that bar a alveolar from producing: a solar with enlisted incompatibility tadalafil 5 mg professor jacket to also be everyday of the thousandfold how much violator is in each exclusive and whether it is blown

  Reply
 3. DennOl

  but there are also medicate for twopence generic viagra that bar a alveolar from producing: a solar with enlisted incompatibility levitra 20 To-do out of the closet any of these bellies lower for the benefit of studios

  Reply
 4. Julian Marean

  Thank you for the sensible critique. Me and my neighbor were just preparing to do some research about this. We got a grab a book from our local library but I think I learned more from this post. I am very glad to see such great info being shared freely out there.

  Reply
 5. sirgliofrei

  It is perfect time to make some plans for the future and it’s time to be happy. I’ve read this post and if I could I want to suggest you few interesting things or suggestions. Maybe you could write next articles referring to this article. I desire to read even more things about it!

  Reply

Leave a Reply

Your email address will not be published.